Uzuri na utulivu wa misitu hakika ni kivutio kwa kila mmoja wetu. Licha ya utunzaji wa viumbe mbalimbali zaidi ya nane kwenye msitu. Bado msitu ni mhimili wa maisha ya kila siku ya binadamu. Hivyo basi kila mmoja wetu inampasa kuchukua hatua pale inapogundulika kuwa kuna uharibifu.

Licha ya kuonekana kuwa msitu ni mhimili na ni kichocheo cha maisha bora ya mwanadamu ya kila siku. Lakini bado kuna vitisho vikali dhidi ya misitu, hususani kwa ajili ya matumizi ya kilimo kutokana na ongezeko la idadi ya watu na mabadiliko ya uhitaji wa chakula lakini hata ukataji usio halali kwa shughuli za binadamu.

Msitu ni nini?

Msitu ni mkusanyiko wa uoto asilia unaojumuisha miti mingi ya aina mbalimbali kwa mfano mipingo, mikoko n.k. lakini pia mimea na nyasi ambazo huweza kuwa fupi au ndefu. Misitu inaweza kuwa ya asili ambayo huota yenyewe bila kupandwa na binadam au isiyo ya asili yaani ya kupandwa na binadamu.

Uhifadhi na matumizi halali ya misitu

Kutokana na uwepo wa uharibu mkubwa wa misitu unaojumuisha ukataji usio wa halali wa miti, shirika la WWF (World Wildlife Fund)  linalohudumia Misitu na viumbe hai la kimataifa ambalo linafanya kazi kwenye zaidi ya nchi 100 Duniani wakishirikiana na CARE walitembelea Mkoani Lindi kwenye Wilaya ya Nachingwea kwa ajili ya kutoa mafunzo ya utunzaji wa misitu.

SOMA ZAIDI:

Wakiwa chini ya uratibu wa True Vision Production ambao walihusika katika kuandaa Makala mbalimbali za video. Wanakijiji waliweza kupokea Mafunzo ambayo yalijumuisha uchoraji wa ramani ya misitu yote wilayani humo kabla ya kutoa mafunzo halisi kwa baadhi ya vikundi. Mafunzo hayo yalijikita hasa kwenye

  • Uvunaji wa Miti
  • Kutambua thamani ya miti kwa Cubic Meter
  • Kukokotoa gogo
  • Kujua ujazo wa Ubao mmoja

M

“kwakuwa sikuwa na elimu yeyote nilichokuwa naangalia nikate miti, nipasue mbao niuze maisha nyumbani yaende”-Alisema bwana Omary Mbuda, mmoja wa wanakikundi kilichopokea mafunzo ya uvunaji wa miti Wilayani Nachingwea.