Kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana kwa nchi za Tanzania, Rwanda, na Msumbiji, ni mara 2-3 zaidi kuliko cha watu wazima. Lakini pia kuna kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira kwa wanawake wenye umri mdogo. Hii ni kwa mujibu wa takwimu za shirika la kimataifa lisilo la kibiashara la Maendeleo la nchini Uholanzi (SNV)

Zaidi ya hayo, viwango vya umaskini katika nchi hizi tatu vinatoka 45% hadi 68%, kulingana na Benki ya Dunia. Wengi wa vijana wa vijijini wanategemea ajira ya “hatari” katika kilimo cha kujiendeleza. Pamoja na kazi isiyo rasmi ya kujitegemea bila ya mapato imara au fursa ya maendeleo ya kitaaluma au ukuaji wa muda mrefu.

Kwa hiyo, vijana wengi wa vijijini huhamia mijini kutafuta kazi, lakini mara nyingi hawana ujuzi wa kutosha au kuelewa wazi mahitaji ya soko.

UTEKELEZWAJI WA MRADI WA OYE

SNV inatekeleza mradi wa OYE (Opportunities For Youth Employment) nchini Rwanda, Tanzania na Msumbiji kwa lengo la kuboresha maisha ya vijana wa vijijini, wa nje wa shule ya 27,050 kwa njia ya mafunzo ya ujuzi kwa njia ambayo huchochea matarajio yao wenyewe na mahitaji ya kilimo cha ndani, nishati mbadala, biashara na usafi wa maji.

Nchini Tanzania Shirika la viwanda Vidogo vidogo (SIDO) limekuwa likitekeleza mradi huu, majukumu yake yakiwa ni kutafuta vijana na kuwafundisha mafunzo mbalimbali kulingana na matakwa ya  Mradi wa OYE.

Bi Elizabeth Rogers Barnaba ni mkazi wa Dodoma nchini Tanzania na yeye ni mmoja ya wanufaika wa mradi wa OYE kupitia SIDO. Kabla ya kujiunga na mradi huu Bi Elizabeth alikuwa akifanya kazi kama katibu kwenye kampuni ya Mawakili. Kwa sasa ana kikundi rasmi kijulikanacho kwa jina la Haki Leather Products.

Bi Elizabeth anasema kwake Mradi huu wa OYE kupitia SIDO umemuwezesha kujua mfumo mzima wa stadi za maisha. Ikiwemo na kupata ujuzi wa namna ya kuanzisha na kufanya biashara pamoja na kujitambua kama kijana.

SOMA ZAIDI:

Kazi za SIDO kwenye mradi wa OYE

  1. Kutafuta vijana na kuwapa mafunzo

SIDO kama muendeshaji wa mradi huu jukumu lake kubwa ni kutafuta vijana na kuwapa mafunzo yanayoendana na matakwa na malengo ya mradi husika wa OYE.

  1. Kutoa Elimu kuhusu kubuni na kuaandaa mipango ya biashara

Moja ya mafundisho ambayo hutolewa na SIDO kupitia mradi wa OYE ni kufundisha elimu ya biashara. Namna ya kubuni biashara husika pamoja na kuandaa mipango kazi ya ufanyaji wa biashara husika.

  1. Kutoa elimu ya kujitambua kwa vijana

Vijana wakiwa ndio walengwa wakubwa wa mradi wa OYE kabla ya SIDO kuwaingiza kwenye mfumo maalumu. Vijana hawa upewa elimu ya kujitambua kama kijana na kuona fursa ya biashara ili kuweza kufanya biashara kwa ufanisi.

  1. Ujuzi

Ujuzi ndio suala zima ambalo linaakisi maana nzima ya mradi wa OYE. SIDO utoa ujuzi mbalimbali kwa vijana ili kuweza kujiajiri wenyewe. Kupitia fani mbalimbali SIDO huwapa motisha vijana waliopata ujuzi kutumia vifaa vya SIDO kwa ajili ya kubuni na kutengenza bidhaa zao.

  1. Kutoa Elimu kuhusu taarifa za Masoko

Ujuzi na kujitambua unaweza kutengeneza kitu kinachoweza kukuingizia kipato. Lakini bila kuwa na uelewa wa wapi bidhaa yako unaipeleka na kuipeleka kwa namna gani bado haitakusaidia kitu. SIDO utoa elimu kuhusiana na taarifa za Masoko kwa vijana lengwa kwenye mradi wa OYE.

True Vision Productions kupitia Ubalozi wa Uswisi chini ya wakala wa Maendeleo na ushirikiano Uswisi, ndio waliofanikisha kuandaa makala mbalimbali za wanufaika wa mradi wa OYE kupitia SIDO nchini Tanzania.

Mradi wa OYE unaotekelezwa na SNV kwa kushirikiana na Foundation ya Mastercard na Shirika la Uswisi la Maendeleo na Ushirikiano Uswisi, umekusudia kuwafikia vijana wasiokuwa na ustawi wa vijijini wenye umri wa miaka kati ya miaka 18 na 24, angalau 40% kati yao ni wanawake wenye umri wadogo.