Uzalishaji wa maudhui yaliyo kwenye mtindo wa Video (Picha mjongeo) kwa sasa unaonekana kushika kasi mno kwa kipindi cha hivi karibuni. Hii inatokana na uhitaji mkubwa wa maudhui ya picha mjongeo. Ambapo hutumika katika shughuli mbalimbali kama vile kufuta masokoa kibiashara pamoja na shughuli mbalimbali za kijamii.

True vision Production wamekuwa wakijikita sana kwenye wigo huu hasa katika kuboresha vitendea kazi pamoja na rasilimali watu wenye kukidhi mahitaji ya shughuli nzima ya uaandaji wa vipindi mbalimbali vilivyo kwenye maudhui ya video (Video Content).

Vipo vipindi mbalimbali vinavyoandaliwa na True vision kutoka eneo husika la mradi lakini pia matukio ya moja kwa moja (Live) kutoka kwenye eneo husika au shughuli husika kwa ajili ya kuwapa taarifa watu kwa njia ya video.

Uhodari pamoja na weledi wa waandaji wa vipindi mbalimbali vya Televisheni unawafanya True vision Production kushiriki kwenye miradi mbalimbali ya ndani na nje ya nchi hasa katika kitengo ya uandaaji wa makala pamoja na urushaji wa matangazo ya moja kwa moja kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile YouTube, Instagram n.k

Lakini pia, matumizi ya vifaa vyenye kuwa na sifa ya kupata picha mjongeo kutoka kwenye mazingira mbalimbali kama vile maeneo ya chini ya maji (Under water film). Hii pia inawapa nguvu kama moja ya kampuni zilizojidhatiti katika sekta ya uandaaji wa maudhui yaliyo katika mtindo wa Video (Video Production)

Ili uweze kutazama makala na vipindi mbalimbali vilivyoandaliwa na True vision Production (TVP), tafadhali tembelea akaunti ya Youtube ya TRUE VISION PRODUCTION.