Elimu kwa maana pana ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine.

Ni wazi jamii inahitaji elimu ili kuweza kujikomboa katika nyanja mbali mbali ikiwemo kiuchumi, utamaduni na hata kijamii. Elimu ndio msingi wa maisha ya bianadamu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu.

Elimu ni urithi maridhawa kutoka kizazi hadi kizazi. Licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta hii. Lakini bado jamii na viongozi wa sekta husika wanafanya kila linalohitajika ili kuhakikisha tunajikomboa kutoka kwenye changamoto hizo.

Hakielimu

SOMA ZAIDI:

HAKIELIMU

Mchango wa True Vision Production Kwenye Sekta ya Elimu

True Vision Production (TVP) nao hawako nyuma. Kwa kipindi cha muda mrefu TVP imekuwa ikifanya kazi bega kkwa bega na wadau wote wa elimu katika kuhakikisha changamoto zinazoikumbuka sekta ya elimu zinapungua kama si kuondoka kabisa. Moja ya wadau ambao wamekuwa wakifanya kazi pamoja na TVP ni pamoja na Haki Elimu.

Kupitia Haki Elimu, TVP imekuwa ikifanya miradi mbalimbali inayowalenga wahusika wote wa sekta ya Elimu wakiwemo waalimu pamoja na vitendea kazi.

True Vision production inatoa fursa kwa wadau wa sekta Mbalimbali katika kuhakikisha inamulika changamoto na mafanikio ya sekta husika pale inapohitajika katika hali ya kiwango cha juu zaidi. Hili kuweza kuwasiliana na TVP, tafadhali bonyeza HAPA kwa maelezo zaidi.