Semina zilizoandaliwa na Kampuni ya True Vision Production (TVP) kwa kushirikiana na UNICEF Tanzania na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto za kampeni ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ kwa wahariri, viongozi wa dini na waandishi wa habari zimemalizika katika Hotel ya Regency, jijini Dar es Salaam.

Semina hizo zilikuwa na lengo la kuelimisha makundi haya matatu (wahariri, viongozi wa dini na waandishi) juu ya umuhimu wao wa kushiriki katika kampeni ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.

Tahseen Alam, Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka UNICEF Tanzania

Tahseen Alam, Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka UNICEF Tanzania amesema serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau imekuwa ikifanya jitihada kubwa katika miaka 10 iliyopita ya kuokoa vifo vya mama na mtoto, ikiwemo eneo la chanjo ambapo watoto wengi na mama wajawazito wanapatiwa.

Lakini kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mtaalamu wa Mawasiliano mwenzake kutoka UNICEF, Usia Nkoma, Tanzania bado ina safari ndefu ya kutokomeza vifo hivyo kwa sababu ni nia tisa kati ya nchi 10 duniani zinazoongoza kwa vifo vya mama wajawazito na watoto.

Takwimu zinaonyesha mama wajawawanakufa kila mwaka wakati wanajifungua, sawa na wanawake 312 kila siku.

Pia asilimia 50 ya watoto walio chini ya miaka mitano (5) pia wanakufa ndani ya mwezi mmoja baada ya kuzaliwa, asilimia 40 kati ya hawa wakiwa watoto wachanga.

Mwandishi na Mhariri mkongwe nchini, Theophil Makunga

 

Wakizungumza tofauti tofauti katika semina hizi, mmoja wa waandishi na wahariri wakongwe nchini, Theophil Makunga amasema takwimu hizi zinatisha, hivyo kuna haja kwa wahariri kuzipa kipaumbele habari zinazohusu wanawake wajawazito na watoto ili kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuchukua hatua kupunguza vifo hivi.

Sheikh Hamid Jongo wa msikiti wa Manyema kariakoo dar es salaam

Naye Sheikh Hamid Jongo wa msikiti wa Manyema amesema kuna haja ya kuwafunda watumishi wa afya , kwani baadhi yao hawana lugha rafiki kwa wagonjwa.

Mchungaji Christosiler Kalata akichangia hoja latina semina ya Jiongeze Tuwavushe Salama, yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga vinavyotokana na uzazi

Kauli yake imeungwa mkono na Christosiler Kalata, mchungaji kutoka KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, ambaye amehimiza maadili ya kazi kuzingatiwa na jamii kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika kampeni ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ ili kuhakikisha vifo vya mama wajawazito na watoto vinaisha.

“Tutahakikisha, kama waandishi wa habari tunabadili mtazamo wa kazi zetu kwa kuzipa kipaumbele habari zinazohusu afya ya mama wajawazito na watoto, kama ilivyo kwa habari nyingine,” amesema Tumaini Msowoya, kutoka gazeti la Mwananchi.

UNICEF,wawakilishi wa wizara ya afya na Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali tanzania

Washiriki wote wameishukuru kampuni ya True Vision Production, UNICEF Tanzania na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto kwa kwa kuhakikisha kampeni ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ inafanikiwa, kwani jukumu la kupunguza vifo na kila mmoja katika jamii.

Bonyeza hapa kwa maelezo zaidi