Musa Mbwego, a.k.a Kaka Musa akifanya yake katika moja ya majukumu yake ya kikazi

Ukiwa mpenzi wa burudani, basi lazima utakutana na kazi zilizopitia katika mikono ya Kaka Mussa, jina analojulikana zaidi katika kazi zake za kuzalisha kazi za video (video production), kupiga picha na kurusha drone kwa ajili ya kuchukua picha za juu.

Na kadri siku zinavyokwenda, ujuzi wake unazidi kukuwa na sasa hivi Kaka Musa, au Musa Mbwengo kwa jina lake la kuzaliwa, anafanya kila aina ya kazi inayohusiana na video production.

Musa Mbwego (kushoto) akiwa ni sehemu ya crew ya Maisha Plus

Tamasha la Wasafi Festival na matukio yote ya Wasafi yanayofanywa mubashara (live) na mengine mengi ni moja ya kazi zinazomtambulisha Mbwego katika tasnia ya video production, akiwa kama Muongozaji msaidizi (Assistant director).

Akiwa anafanya kazi zake kwa kujitegemea (freelancer), Mbwego kwa wakati tofauti tofauti anafanya kazi za video na kampuni nyingi kama vile Studio19, Take2 Production, Bench Mark, DMP (Maisha Plus) na True Vision Production (TVP) pale anapohitajika.

Anasema si rahisi kukubalika na kampuni zote hizi, wakati mwingine anajikuta anahitajika huku na kule, lakini ufanyaji kazi kwa kujituma na nidhamu ya hali ya juu ndio siri yake.

Waswalini wanasema ukiona kinaelea, ujue kimeundwa. Mbwego anasema kujulikana kwake na kufanya kazi na makampuni/watu mbalimbali kusingekuwepo kama isingekuwa TVP.

TVP imemfungulia dunia kuwa alivyo hivi sasa na kuweza kufanya kazi pia na mashirika makubwa kama zile USAID, CNN na Google, akisafiri sehemu mbalimbali na kufanya kazi tofauti tofauti.

Urushaji wa drone kwa ajili ya kuchukua picha ni moja ya kazi inayomfanya kaka Musa ajulikane zaidi, kama anavyoonekana pichani. Wengine wanamuita Musa Madrone.

Anasema kama isingekuwa TVP, Mbwego anayejulikana leo si ajabu angekuwa akifanya kitu kingine tofauti, kama sio kufanya kazi za teknolojia ya Habari (Information Technology-IT) aliyoisomea akiwa Arusha.

Anasema wakati akiwa Arusha mwaka 2004, TVP, ikiwa kampuni changa wakati huo, ilikuwa inataka mtu anayeweza kufanya kazi za IT na masuala ya kutengeneza video (video production).

Mbwego anasema alifanikiwa kujiunga na TVP, licha ya kuwa na uelewa mdogo wa kazi za video production, akiwa na imani ya kujifunza zaidi akiwa kazini na moja ya kazi alizoanza kufanya ni kuhariri kazi za video (editing), ikiwa ni mara yake ya kwanza kutumia komputa aina ya MAC kwa wakati huo.

Kadri siku zilivyoenda naye alikuwa anajifunza zaidi chini ya mkurugenzi David Sevuri, ambaye alimfundisha vitu vingi vinavyohusiana na video production.

“Niliweza kufanya kazi nyingi, kama vile kuhariri matangazo ya Haki Elimu na kurekodi Voice Over (kuingiza sauti) katika matangazo,” anasema Mbwego.

“ Vifaa kama Crane, Dolly vikaanza kununuliwa TVP miaka hiyo ili tuvitumie katika kazi zetu,”
“Sevuri alitaka sana tujifunze na pale alipoweza, alinunua vifaa vinavyohitajika

“Aliumia sana vifaa vilivyonunuliwa visipotumika ipasavyo kwa sababu alitaka watu wajifunze na tuliweza kujifunza vitu vingi sana,” anasema Mbwego.

Katika maisha yake ya kazi, Mbwego alifanya kazi nyingi sana toka alipojiunga mwaka 2004 mpaka mwaka 2011 alipoondoka TVP ili akafanye kazi kama freelancer, akiamini ameiva katika idara zote.

“Niliingia TVP nikiwa miongoni mwa wafanyakazi wachache wa kwanza kabisa mpaka leo hii naiona (TVP) ikiwa imepiga hatua kubwa na kutumia vifaa vya kisasa kabisa vya Video Production,”

“Ndio maana, kwa kuwa niliondoka vizuri, mpaka leo hii bado nafanya kazi za TVP pale ninapohitajika na kujifunza zaidi, kikazi na kiteknolojia,”anasema baba wa watoto watatu.

Kuweza kurusha drone katika uchaguzi wa Raisi Tanzania, kurusha mubashara vipindi vya Maisha Plus Season 3 na Tamasha la Fiesta na kazi nyingine nyingi ni miongoni mwa kazi zilizompa moyo kuwa anaweza na kuthubutu kumuomba Sevuri aondoke TVP ili akajaribu maisha yake binafsi ya kikazi.

Hii ni kwa sababu Mbwego anasema ana ndoto ya kuwa na ‘Production House’ yake katika siku za usoni Mungu atakapomjaalia.

Anasema moja ya vitu anavyovikumbuka akiwa kazini ni ukali wa Sevuri, ambaye hakutaka watu washindwe kitu.
“Alikuwa rafiki sana nje ya kazi, lakini wakati wa kazi alikuwa mkali kwa sababu Sevuri hakuwa na msamiati wa kushindwa tunapokuwa field,” anasema Mbwego.

“Ni mtu ambaye anajiweka kikawada sana pale mnapokuwa field, akikubali ushauri wa wengine,”
“Tunafanya kazi kama team-bila ya kujali yeye ni bosi,”
“Hii imenipa funzo la kuishi na watu kirafiki na kikawaida sana ili uweze kupata ushirikiano,” anasema Mbwego.

Lakini pia kuwa na nidhamu ya kazi na kufanya kazi kwa wakati ni moja ya vitu vingine vingi alivyojifunza kutoka kwa Sevuri na wanfanyakazi wenzake.

“Leo hii nafanya kazi kubwa sana kwa sababu TVP imekuwa ni zaidi ya Production House kwangu, ni chuo cha kazi kinachozingatia weledi, ambacho kimezalisha vijana wengi sana walio katika production house mbalimbali na kwenye vyombo vya habari,” anasema Mbwego.

“Hivi karibuni nilikuwa Zanzibar nikifanya kazi na Google Map (Street V iew) kwa ajili ya kuiweka katika ramani mitaa ya Zanzibar kwa kutumia drone.

“Lakini niliwahi pia kufanya kazi na CNN kwa kutengeneza video (nikiwa cameran) wa video zilizohusu Ujasiriamali na USAID kutengeneza video zenye kuelezea mafanikio (success stories) za masuala yanayohusu uzazi na watoto,” anasema Mbwego.

Mbwego anasema licha ya kuwa ameondoka TVP mwaka 2011 akiwa kama mfanyakazi, lakini bado anajiona ni sehemu ya kampuni hiyo.

“Mimi bado ni sehemu ya TVP kwa sababu imenipa heshima katika kazi zangu,”
“Ndio maana pale nipohitajika TVP wakati wowote nakwenda kwa sababu imenifungulia milango,”
“Lakini mimi pia nimekuwa ni sehemu ya kuwafundisha vijana wengine ili nao wajifunze kile nilichojifunza mimi TVP,”.anasema Mbwego.

Anawashauri vijana wanaochipukia katika tasnia ya Video Production kuwa na ari ya kujifunza zaidi kwa sababu teknolojia imekuwa sana na wanahitajika kuwa wabunifu ili waweze kuzalisha kazi nzuri na kuingia katika soko la ushindani.

Am hakika True Vision Production (Video Production in Tanzania) ni shamba na wengi waliolima mavuno yao hakika yanauzika duniani kote. Unaweza kuwasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA ama kwa kufika ofisini kwetu kwa kazi yeyote inayohusiana na Video (Makala, kampeni, na miradi mbalimbali.)