Inakadiriwa kuwa zaidi ya watoto Milioni 250 Duniani kote wanaotoka kwenye mazingira duni hawajui kusoma, kuandika na hata kuhesabu. Idadi inayokadiriwa kuwa ni zaidi ya robo ya watoto ambao hawajui kusoma, kuandika wala kuhesabu.

Kwa mujibu wa tafiti za shirika linalojihusisha na elimu, UNESCO, 1 kati ya watoto 5 Duniani anashindwa kwenda shule, huku ikionyesha uhitaji wa walimu milioni 68.8 Duniani kwa ajili ya kutoa elimu ya msingi kwa kila mtoto ifikapo mwaka 2040.

Xprize

SOMA ZAIDI:

Global learning Xprize nchini Tanzania

Nchini Tanzania Global learning Xprize ilizunguka kwenye vijiji zaidi ya 170 ambapo zaidi ya watoto wapatao 3000 wasiojua kusoma, kuandika na walifikiwa na kupatiwa tables yenye kufundisha kusoma, kuandika na kuhesabu katika lugha ya Kiswahili.

True Vision Production (TVP) ni moja ya kampuni ya Uzalishaji wa Makala zaa Video mbalimbali Duniani. Kampuni ambayo ilipata nafasi ya kuandaa Makala ya mradi huo kwenye vijiji mbalimbali nchini.

Kabla ya kuanza kwa mradi huu (Global learning xprize) nchini Tanzania. Utafiti wa kwenye vijiji vilivyofikiwa unaonyesha zaidi ya 74% ya watoto walioshiriki wanaripotiwa kutopata elimu kabisa. 80% walikuwa hawana uwezo wa kujifunza hata wakiwa nyumbani. Na 90% walikuwa hawana uwezo wa kusoma hata sentensi moja ya lugha ya kiswahili.

Xprize

Ushiriki wa True Vision Production kwenye mradi

Kwenye hafla ya Utoaji wa tuzo ya Global learning xprize. Kampuni hiyo haikusita kuimwagia sifa kampuni ya True Vision Production kwa uhodari wake wa kutengeneza Makala zenye kusaidia watoto kusoma kwa kutumia tablet Duniani.

Ushiriki wa kampuni ya TVP kwenye sekta mbalimbali umekuwa mkubwa hasa kwenye sekta ya Elimu.

Licha ya kumwagia sifa, kwa upande wa Tanzania TVP ilipata nfasi ya kuingia kwenye shindano la maalumu la Makala za video Duniani ambapo makampuni mawili ya kimataifa yanayojihusisha na utoaji elimu, KitKit ya Korea Kusini na ile ya OneBillion ya Kenya na Uingereza kushinda kiasi cha dola milioni 15 katika tuzo zilizofanyika mubashara (live) nchini Marekani katika ofisi za Google.

Global learning Xprize ilizinduliwa mwaka 2014. Ikiwa na lengo la nkusaidia watoto wapatao milioni 250 Duniani. Watoto wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa kuwapatia vifundisho visaidizi (softwares) ambazo zinawafanya wasome, kuandika na kuhesabu wenyewe kupitia tablets.