Chama cha Maofisa Mawasiliano serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari Maelezo, kiliandaa mafunzo maalumu ya wiki moja yanayolenga sekta ya habari katika kufanya kazi kwa weledi ambayo yamemalizika mjini Dodoma hivi karibuni na kampuni ya True Vision Production (TVP) ilipewa nafasi ya kuwa sehemu ya watoa mada katika mafunzo hayo.

Ushirikishwaji wa TVP katika mafunzo hayo umetokana na umahiri na uweledi wake katika utengenezaji wa kazi za video (Video production) hapa nchini.

Na hii ndio imepelekea TAGCO na Idara ya Habari Maelezo kuishirikisha TVP katika mafunzo hayo ili kubadilishana uzeofu wa utendaji kazi na maofisa hao katika masuala yanayohusu utengenezaji na kuhariri wa vipindi/makala za video.

Mkurugenzi wa TVP, David Sevuri, wakati anawasilisha mada kuhusu utengenezaji na uhariri wa video, aliongelea kuhusu uzoefu wake wa zaidi ya miaka 20 katika utendaji kazi, kitu ambacho washiriki walifurahia sana kwa kubadilishana uzeofu katika mafanikio na changamoto za utendaji kazi alioupitia.

Mkurugenzi wa TVP, bwana David Sevuri akitoa mada kwenye mafunzo maalumu ya wanahabari mjini Dodoma

TVP imekuwa ikifanya kazi na mashirika ya kitaifa, kimataifa/taasisi/makampuni na serikali kwa kutengeneza kazi mbalimbali zinazohusiana na uzalishaji wa kazi za video production, matangazo ya redio na runinga.

Miongoni mwa mashirika hayo ambayo yamekuwa yakifanya kazi na TVP ni World Bank, UNICEF, USAID, Wakala wa Serikali Mtandao (e-GA), CARE International, Uhamiaji na Idara ya Habari Maelezo, ambao waliipa kazi TVP ya kutengeneza documentari ya miaka miwili ya Raisi John Pombe Magufuli tangu alipoingia madarakani.

Uzoefu na weledi wake katika kushirikiana na makampuni/ taasisi/mashirika mbalimbali ndio kumepelekea TVP kuwa sehemu ya watoa mada.

Katika mafunzo hayo ya wiki moja yaliyoanza kufanyika tarehe 2-6 mwezi huu (Desemba), Sevuri aliwasilisha mada hizo katika siku mbili, huku Msemaji Mkuu wa Serikali, Daktari Hassan Abbas akitoa mada zinazohusu maarifa ya uandishi (writing skills) na Mr Kafumba akitoa mada kuhusu mitandao ya habari ya kijamii (social media).

Uwasilishaji wa mada uliwavutia sana washiriki ,huku maafisa habari hao wakivutiwa na kufurahia somo la uhariri ( video editing) ambalo lilifundishwa kwa vitendo na Sevuri pamoja na Stephano Lihedule.

Katika mafunzo hayo Lihedule aligusia hatua nne muhimu za uzalishaji (video production) development, pre-production, production na post production ili kuzalisha video bora zenye maudhui kwa hadhira.