Ni wazi jina la True Vision Production (TVP) si geni kwenye macho na masikio ya walio wengi nchini. Hii ni kutokana na uzalishaji wa kazi mbalimbali zikiwemo za kijamii ambazo zinaakisi maisha ya jamii nzima kwa ujumla. Ni wazi zipo kazi nyingi sana ambazo umezitazama zilizozalishwa na TVP.

Ubora wa kazi pamoja na kujitoa ndio msingi mkubwa wa mafanikio ya kazi za TVP. Lakini pia uwepo wa nguvu kazi yenye yenye uwezo wa hali ya juu na kujitoa pia ni kigezo cha ufanisi. Wakiwa na jopo kubwa la wataalamu kwenye kila idara ya uzalishaji wa picha mjongeo, TVP wana kila sababu ya kujivunia hilo.

Crew ya True Vision Production ikiwa kwenye moja ya majukumu ya siku

SOMA ZAIDI:

Zipo kazi nyingi za True Vision ambazo zimeleta ufanisi mkubwa katika jamii. Kazi kama vile za Haki Elimu, Uhamiaji, hifadhi za Taifa n.k ni moja ya kazi ambazo zimeleta matokeo chanya kwenye jamii yetu. Msingi mkubwa wa kazi hizi ni  kuleta mabadiliko chanya ambayo italeta mapinduzi katika sekta mbalimbali.

Lakini pia upatikanaji wa vifaa mbalimbali vyenye uwezo mkubwa unafanya kazi ya True Vision Production kuwa maridadi na yenye mvuto machoni kwa watu. Ni wazi hivi vyote vinahitaji uwekezaji wake mkubwa. Kwa kuzingatia kuwa na kazi zenye ubora TVP haijawahi kusita kwenye eneo hilo hasa katika uwekezaji kwenye vifaa.

Karibu True Vision Production kwa ajili ya kupata kazi zenye ubora na zenye kubeba ujumbe uliokusudiwa kwa jamii.  Kwa ajili ya kufanya kazi na sisi tafadhali bonyeza HAPA kwa mawasiliano zaidi.