True Vision Production (TVP) ni moja ya kampuni ambayo kwa namna moja imefanikiwa kushiriki kwenye miradi inayogusa sekta mbalimbali nchini. Miradi hii ndio chachu ya maendeleo ya kijamii kwa ujumla. Ushiriki wake umeongeza tija katika kukuza ustawi wa jamii kwa ujumla hasa katika kuongeza uelewa juu ya miradi mbalimbali inayotekelezwa.

TVP imefanikiwa kushiriki katika miradi na kampeni mbalimbali za kukuza uelewa kama vile kwenye sekta ya elimu, afya, nishati, maji, michezo, fedha, uhamiaji, uchumi, kilimo, rushwa, Sanaa, utalii, usafiri hasa wa anga, uvuvi pamoja na masuala ya wanawake na maendeleo.

True vision production, video production company in tanzania

Baadhi ya Miradi katika sekta mbalimbali

Katika sekta ya elimu

True vision production imeshiriki katika kuandaa kampeni mbalimbali zinazolenga kumuinua mtoto kielimu. Lakini pia ushiriki katika kuboresha mazingira ya elimu yatakayomfanya mwanafunzi kupata elimu bora na mwalimu kuweza kutoa elimu stahiki. Lakini pia kuongeza uelewa katika kuwalinda watoto wa shule.

Kwenye sekta ya afya

TVP imeshiriki pia katika kutoa ufahamu juu ya mambo mbalimbali kwa jamii juu ya afya. Mambo haya yanajumuisha masuala ya uzazi, bima za afya, elimu juu ya uzazi, lishe pamoja na umuhimu wa upatikanaji wa vituo vya afya na zahanati.

Sekta ya utalii,

True vision Production imejikita hasa katika kuzimulika kwa kina baadhi ya hifadhi zilizopo nchini. Hifadhi hizi ndizo vivutio vya nchi na ndio chachu ya uchumi wetu. Hifadhi kama Ngorongoro, Serengeti na hata hifadhi nyinginezo.

Katika sekta ya nishati na gesi,

True vision production imejihusisha na uandaaji wa Makala mbalimbali zinzohusiana na upatikanaji wa gesi nchini na fursa zake. Lakini pia upatikanaji wa umeme vijijiji.

Uchumi,

Hii ni sekta inayogusa sekta zote. Kwa kulitambua hilo True vision production ilifanya Makala mbalimbali katika kuiangazia kwa kina sekta hii. Makala hizi ziliangazia hasa katika masuala ya uwekezaji, mifumo ya biashara hasa ya kuvuka miapaka ya nchi kwa baadhi ya vikundi mbalimbali. Na idara mbalimbali za kifedha kama vile benki pamoja na taasisi za kimaendeleo kama vile TASSAF

Masuala ya kilimo

TVP ilijikita katika kumulika miradi mbalimbali inayofanywa na jamii kupitia taasisi mbalimbali kwa vikundi. Kazi kubwa ya TVP ni kuimulika miradi hii ili iweze kuleta changamoto katika jamii pamoja na kuona maendeleo yake.

Hiyo ni baadhi tu ya miradi ambayo True Vision Production imeshiriki kwa namna moja ama nyingine kwa uchache tu. Ushiriki wake sit u kuwa unaleta tija kwa wazabuni wa miradi hiyo bali kuibua changamoto mpya kwa jamii nyingine katika kuiga mfumo mzima wa maendeleo.

Kuangalia miradi mbalimbali iliyoshirika TVP, tafadhali bonyeza HAPA