Siku chache zilizopita taasisi ya The International Tourism Film Festival Africa (ITFF) ilitangaza washindi wa tuzo mbalimbali za utengenezaji wa filamu bora barani Afrika. True vision ndio mshindi pekee kwa upande wa Tanzania miongoni mwa washiriki mbalimbali wa kimataifa waliokuwa kwenye kinyang’anyiro hicho, akishinda tuzo mbili.

Tuzo hizo kwa upande wa True Vision zimetokana na video inayoongelea uzuri wa hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. Tuzo moja ikiwa ni video hiyo kushinda namba moja miongoni mwa video nyingine zilizowasilishwa na washiriki mbalimbali Afrika na huku tuzo nyingine ikiwa ni ya jumla katika kipengele cha Uzuri wa Asili na Maisha ya wanyama mbugani (Nature & Wildlife).

True vision production, video production company in tanzania

Hii ni hatua kubwa kwa True Vision Production katika kujiimarisha kitaaluma na weledi katika tasnia ya utengezaji wa filamu, Makala pamoja na video mbalimbali ulimwenguni. Lakini pia hii inatokaana na utendaji kazi ulio mahiri ikiwa ni pamoja na kutumia rasilimali watu wenye uwezo mkubwa pamoja na vifaa vyenya uwezo mkubwa katika kuzingatia ubora wa kazi husika.

Tuzo hizi zinapangwa kutolewa rasmi mwezi April, 2020 huko Afrika Kusini kwenye sherehe/hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali wa tuzo za ITFF barani Afrika. True Vision Production akiwa mmoja wa washindi hao.

True vision production, video production company in tanzania

Mwisho True Vision Production (TVP) inapenda kuwashukuru watoaji wa tuzo hizi The International Tourism Film Festival (ITFF) kwa kutambua ubora wa kazi zetu, lakini pia wadau mbalimbali waliofanikisha kufanyika kwa Makala mbalimbali ikiwemo hii ya Ngorongoro Crater, lakini wote waliohusika katika uandaaji na utengenezaji wa Makala hii yenye kuelezea uzuri wa asili wa hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro (Ngorongoro Crater)

TAZAMA VIDEO YA NGORONOGORO CRATER HAPA CHINI.