Wiki ya Azaki 2019 imeanza mapema wiki hii ndani ya makao makuu ya serikali, mjini Dodoma. Kama ilivyo kawaida, True Vision Production (TVP) imekuwa ni sehemu ya wadau wa The Foundation For Civil Society (FCS) wakipewa jukumu la kuuhabarisha umma juu ya matukio yote yanayotokea kwa juma moja.

Tukio kubwa lilikuwa maandamano yaliyoanzia katika Viwanja vya Nyerere Square, yakihusisha watu kutoka makundi mbalimbali huku brass band ya JKT ikiwa mbele na matarumbeta. Kwa kweli mji wa Dodoma ulipendeza na kuzizima na sare maalumu na mabango yenye kuonyesha umuhimu wa siku hii ya Asasi za Kiraia nchini Tanzania, inayoandaliwa kwa mara wa pili mfululizo na The Foundation For Civil Society.

True Vision Production, kwa kutumia weledi wake imekusanya matukio yote muhimu kwa kutumia video, picha za mnato na kutengeneza clip ndogo ndogo za siku kwa ajili ya wadau wa mitandao ya kijamii (social media) ili kushea katika platform mbalimbali kama vile Twitter, Instergram, YouTube na Facebook.

TVP, ukiachia jukumu la kila siku, pia itatengeneza documentary maalumu ya tukio lote la wiki nzima ambalo litatoa taswira nzima na malengo ya wiki ya Azaki kwa mwaka 2019.

Midahalo mbalimbali inafanyika katika Hoteli kubwa ya Morena, huku kumbi zaidi ya nne zikihusika kwa siku kwa watu mbalimbali mashuhuri na waliobobea katika mambo ya Asasi, na watunga sera wakishiriki.

TAASISI SHIRIKI

Asasi na taasisi mbalimbali za maendeleo kama vile UN Women, Oxfam, Twaweza, Policy Forum, Msichana Initiative, UNA Tanzania, Sikika, Tango, Tanganyika Law Society na wengine wengi ni sehemu ya washiriki

Akiongea katika hotuba ya ufunguzi iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri siku ya Jumatatu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa alitambua mchango wa asasi hizo katika kuleta maendeleo ya kijamii, huku akijulishwa kuwa zaidi ya shilingi billioni 200 za Kitanzania zimelipwa kodi kwa serikali kuu kwa kipindi kifupi tu kupitia asasi 16 kati ya asasi zaidi ya 10,000 zilizosajiliwa nchini.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kasimu Majaliwa akitoa houtuba kwenye wiki ya Azaki 2019

VIONGOZI MBALIMBALI

Waziri Mkuu alisema serikali inatambua mchango wa asasi za kiraia na kuahidi kuendelea kufanya kazi pamoja kama kauli mbiu ya mwaka huu inavayosema”Ubia kwa Maendeleo:Ushirikiano kama nguzo ya Maendeleo nchini Tanzania.

Pia aliwatumia salamu washiriki wote zilizotooka kwa mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa John Pombe Magufuli, akisema kuwa serikali haina tatizo na uwepo wa asasi, akiongeza kuwa zimekuwa ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Naye Mtendaji Mkuu wa The Foundation For Civil Society (FCS), Francis Kiwanga amesema kulingana na kauli mbiu ya mwaka huu, ana Imani ajenda ya Wiki ya Azaki itawezesha asasi za kijamii kufungua milango ya ushirikiano na serikali, bunge, sekta binafsi na mdau mwingine yoyote wa maendeleo.

Mkurugenzi Mtendaji Wa The Foundation For Civil Society , Francis Kiwanga ( kushoto) akishiriki moja ya mada katika wiki ya Azaki 2019.

Malengo ya Wiki ya Azaki ya 2019 ni:

Kuimarisha mahusiano baina ya wadau wakuu wa maendeleo. Tukio hili linalenga hasa mahusiano ya aina tano.

  1. Kwanza Azaki na Serikali (kuonyesha mchango wa sekta ya Azaki kwenye kuchangia maendeleo).
  2. Azaki na Bunge ( lengo kuonyesha ushiriki na mchakato wa Azaki katika michakato ya kisera.
  3. Lakini pia Azaki na Sekta Binafsi ( lengo ni kuongeza mchango wa kifedha na kiufundi katika shughuli za kimaendeleo)
  4. Azaki kwa Azaki (lengo ni kuwajengea sauti ya pamoja na kuwawezesha kufikia malengo ya kuleta maendeleo kama kikundi kimoja.
  5. Azaki-Wananchi (lengo ni kuwawezesha sauti wananchi, hasa wale walio pembezoni kuwa na ushawishi katika michakato ya utawala katika ngazi zote.