Moja ya malengo ya maendeleo ya Milenia yaliyowahi kuwekwa ni pamoja na usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake. Kiujumla lengo hili lilikuwa linataka wanawake au akina mama wapewe fursa sawa katika nyanja zote ikiwamo kiuchumi, kisiasa na hata kijamii.

Licha ya malengo hayo kufikia ukomo wake 2015, lakini bado juhudi zinafanyika ili kuwakomboa akina mama na kuwahusisha katika mfumo mzima wa uzalishaji. Na hii ndio zana ya fursa sawa katika kukuza uchumi.

True Vision Production imetembelea akina mama kutoka katika moja ya mpaka wa Tanzania na Kenya, Holili, Rombo mkoani Kilimanjaro, ambao wamekuwa wakipokea semina mbalimbali kutoka kwenye mashirika mbalimbali hususani kuhusiana na ujasiriamali.

Moja ya mashirika hayo ni pamoja na Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC), ambao walijihusisha na kutoa elimu ya ujasiriamali, SIDO ambao walitoa elimu ya vitendo iliyowawezesha akina mama hao kuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa kama vile,

  • Wine ya rosella
  • Juisi ya Ndizi
  • Unga wa Ndizi
  • Lishe inayotokana na maharage ya Soya (Soya beans). n.k

Hizo zote ni baadhi ya bidhaa ambazo akina mama hao walikuwa na uwezo wa kuzalisha na kuziuza sehemu mbalimbali. Lakini changamoto ya kuuza bidhaa zao haikuwa ndogo kama ilivyodhaniwa hasa ukiangalia soko lao lililenga pia kuuza nje ya mipaka ya Tanzania husani eneo la karibu yao, Kenya.

SOMA ZAIDI:

Changamoto walizopitia katika kuvusha bidhaa zao kwenda Kenya

Soko la nje hususani kenya kwa akina mama wa Holili lilikuwa linawapa manufaa makubwa mno licha ya wao kukiri kuwa hawakuwa na uwezo wa kulipia vibali vya kuvuka mpaka. Hivyo hawakuwa na namna zaidi ya kutafuta mbinu za kuweza kuvuka kwenye mipaka pasipo kutumia utaratibu maalumu (njia za panya). Zipo changamoto walizokutana nazo wakiwa wanavuka mpaka kwa njia za Panya.

  1. Kukamatwa na kutumikia vifungo.

Licha ya akina mama kukiri kuwa walihitaji sana kuuza bidhaa zao Kenya lakini hofu kubwa ilikuwa ni kukamatwa na askari. Wapo waliosadikika kukamatwa mara baada ya kugundulika kuvuka pasipo kuwa na kibali na hatimaye kupewa vifungo.

  1. Kuombwa rushwa

Kwa wao wanasema kutoa rushwa ilikuwa ndio njia mbadala ya kuepuka vifungo. Hivyo akina mama hao wakati mwingine uamua kutoa rushwa ili kujikwamua licha ya kukiri kuwa kipato cha biashara yao kilikuwa kidogo.

  1. Kutoa rushwa ya Ngono

Akina mama pia wanakiri kuna wakati huwa wanalazimika kutoa rushwa ya ngono ili kuweza kujinusuru. Askari anapomakata basi umuomba rushwa ya ngono ili kuweza kumkwamua kwenye kifungo.

Hizo zote ni changamoto ambazo akina mama wamekuwa wakikumbana nazo katika harakati za kuendesha biashara zao. Adha hii kwa sasa akina mama wanakiri kuwa imeondoka kabisa hasa mara baada ya ujio wa TradeMark East Africa.

Mchango wa TradeMark East Africa kwa akina mama wajasiriamali wa Holili

Kazi kubwa ambayoTradeMark wamekuwa wakiifanya kwa akina mama hao ilikuwa ni kufundisha na kutoa elimu itakayowawezesha kufanya biashara yao kwa uhuru. Hii ni pamoja na kufuata taratibu na sheria ya jinsi ya kuvuka mpaka bila usumbufu. Lakini pia elimu ya uzalishaji na ufungaji wa bidhaa zilizo bora.