Tanzania inatajwa kuwa ni moja ya nchi barani Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa sana. Tangu mwaka 2017 kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania ni zaidi ya asilimia 7. Akina mama nao utajwa kama sehemu kubwa inayotumika katika uzalishaji.

Kwa kipindi kirefu kumekuwa na harakati za kupigania usawa wa kijinsia hata katika sekta mbalimbali za kiuchumi. Awali akina mama walitajwa kuwa nyumba tofauti na akina baba katika kutengeneza uchumi endelevu.

Kwa kuzingatia changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwaacha nyuma, taasisi na makampuni mbalimbali sasa yanawatumia akina mama katika njia za uzalishaji pamoja na shughuli mbalimbali za kuongeza kipato, ili waweze kuendesha familia zao.

Shirika la World Wildlife Fund (WWF) wakishirikiana na CARE International wameamua kuzindua mpango maalumu wa uwekezaji wa hisa kwenye vikundi mbalimbali kwa wakaazi wa vijiji mbalimbali nchini, ikiwemo kijiji cha Mbondo, Wilayani Nachingwea mkoa wa Lindi.

akakina mama nachingwea

SOMA ZAIDI:

True Vision Production, iliambatana bega kwa bega na mashirika hayo mpaka katika kijiji cha Mbondo huko Nachingwea kama waratibu wa mradi huo na kuandaa Makala yenye kuonyesha uhalisia wa akina mama wa Mbondo na Familia zao katika mapambano ya kujikwamua kiuchumi.

Kupitia Vikundi mbalimbali kama vile Village Savings and Loan Association (VSLA), familia mbalimbali zimenufaika ambapo kila mwanachama inampasa kuweka hisa inayoanzia shilling elfu moja kwa hisa moja. Moja ya wanufaika wakubwa ni akina mama ambao sasa wanaweza kuchangia gharama za kuendesha familia zao.

Kupitia vikundi hivyo akina mama na wanachama wengine hupokea mafunzo mbalimbali kutoka kwa WWF wakishirikiana na CARE International. Kati ya mafunzo hayo ni pamoja na mafunzo ya,

  • Uchangia wa fedha kwa vikundi
  • Namna ya kujikwamua kimaisha kupitia vikundi hivyo vya hisa.

Bi. Melania Nandonde ni moja ya akina mama ambao wamenufaika na mpango huo wa VSLA. Ambapo kwa sasa anakiri kabla ya kuja kwa mpango wa WWF wa kuanzisha vikundi maisha yao yalikuwa hafifu.

kabla ya vikundi maisha yangu tulikuwa tunalima mimi na mume wangu, tunapata chakula, lakini nyumba yetu tulikuwa tumejenga kwa kutumia nyasi, ilikuwa inafikia usiku mvua zikinyesha nyumba inavuja mno. Kupitia kikundi nasomesha watoto na nimejenga nyumba”-Alisema Bi. Melania

akina mama nachingwea

Mikakati ya kuwakomboa akina mama na familia zako kutoka kwenye uchumi wa chini na kwenda uchumi wa kati ni endelevu. Makampuni na mashirika mbalimbali sasa hufanya kazi bega kwa bega na akina mama katika kuhakikisha familia zinabaki kuwa salama kiuchumi.