A cross-section of a religious leaders at a seminar

Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka UNICEF, Usia Nkoma amesema kujifungua haipaswi kuwa ni chanzo cha kifo kwa mama mjamzito au mtoto atakayemzaa, bali iwe furaha kwa familia.

Akizungumza katika semina iliyohusisha viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali juu ya kuzuia vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga, Nkoma amesema uzazi haupaswi kuwa ni suala la kutabiri kufa au kupona kwa mama anayetaka kujifungua, bali unatakiwa uwe jambo lenye baraka kwa familia kutegemea mama arudi nyumbani salama na kichanga chake.

“Inapaswa kujiuliza tunakosea wapi kwa sababu kujifungua ni kitu cha kawaida (natural process), halipaswi kuwa la kufikiria kufa na kupona, linatakiwa liwe jambo jema lenye kuleta furaha,” amesema.

“Ndio maana kuna haja ya kuhakikisha mama mjamzito na kitoto chake kichanga hawafi kutokana na matatizo ya uzazi ambayo yanaweza kuzuilika ikiwa hatua za makusudi za kuhamasisha wajawazito kwenda kliniki zitachukuliwa,” amesema.

Amesema kuna haja pia ya kuzingatia uzazi salama, kwa mama kuwa na wakati wa kupumzika badala ya kuzaa mfululizo.

Agnes Mgaya, Kaimu Mratibu wa Huduma ya Afya kwa mama na Mtoto mkoa wa Dar es Salaam akitoa mada katika semina ya kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama mama wajawazito na watoto wachanga

Kwa mujibu wa Agnes Mgaya, Kaimu Mratibu wa Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto mkoa wa Dar es Salaam, mama anapaswa kuwa chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya kwa takriban masaa 42 baada ya kujifungua ili aweze kuhudumiwa pindi anapopata changamoto

“lengo ni mama ajifungue salama na kichanga chake kikue salama”,

“Tunataka kuona watoto wanazika wazazi wao, sio wazazi wazike watoto katika umri mdogo”.

Viongozi wa dini mbalimbali, wawakilishi wa UNICEF na Wizara Ya Afya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya semina ya Jiongeze Tuwavushe Salama.

Agnes Mgaya akiongea katika semina