mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa tano kutoka kushoto) na mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga (wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na team ya TVP

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ameisifu kampuni ya True Vision Production (TVP) ya jijini Dar es Salaam kwa kufanya kazi za kutengeneza documentary na matangazo ya video na radio katika ubora wa hali ya juu.

Kazi iliyoifa sifa TVP ni documentary inayoelezea ‘Fursa za Uwekezaji katika mkoa Mchanga wa Simiyu’, ulioundwa mwaka 2012, baada ya kukatwa sehemu ya mkoa wa Shinyanga .

Akizungumza ofisini kwake, Bariadi, mkoani Simiyu, alipotembelewa na timu ya TVP, Mtaka amesema documentary hiyo, inayojulikana kama ‘ Simiyu Investment Guide’ imeitangaza nchi kwa ujumla kutokana na kufanywa katika ubora wa hali ya juu na imetafsiriwa katika lugha za Kiswahili, Kichina na Kiingereza.

Hii imepelekea documentary hii kuwa bora kwa mujibu wa Mtaka na kutumika katika ofizi za balozi nyingi za Tanzania kama sehemu ya kuvutia wawekezaji kuja Tanzania kuwekeza.

“Balozi zetu nyingi zinaitumia documentary hii kuitangaza nchi katika sekta ya uwekezaji,”

“Kwenye Forum ya Mkutano wa China, mheshimiwa balozi wetu wa China Mbelwa Kairuki aliomba iende documentary hii kwa ajili ya maonesho,” anasema Mtaka.

“Hii documentary imekuwa viewed (imeonekana) sana na watu wengi walidhani imetengezwa na watu wa nje kutokana na kasumba mbaya ya kutojali vitu vinavyotengenezwa hapa nchini,” Mtaka ameongeza.

‘Wengi wanaamini vitu vizuri vinatoka nje tu, lakini kupitia documentary hii, tumepata utambuzi (recognition) kutoka kwa serikali, wajasiriamali, vijana na taasisi za kitafiti na zile za kutunga sera  pamoja na vyuo vikuu ambavyo wameingalia,”

“Kila wakati watu wametamani kuangalia na kutuuliza nani ametengeneza na mikoa mingi wameiomba ESRF kutengeneza documentary hii kama yetu,”

“Hata Simiyu tunafaidika na documentary hii, sasa hivi wawekezaji wanakuja Simiyu na tunajenga viwanda mbalimbali, kikiwemo cha kutengeneza bidhaa zitokanazo na pamba ikiwemo diapers (pampers) chenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 7 na viwanda vingine vipo katika michakato,” amesema Mtaka.

Documentary ya Simiyu, iliyofanywa na TVP kupitia Economic and Social Research Foundation (ESRF), inaonyeshwa katika balozi za Tanzania zilizopo nchini Afrika ya Kusini, China, Uturuki, Nairobi, Israel na baadhi ya balozi nyingine.

Mtaka amesema wanategemea kutengeneza documentary nyingine na wataomba TVP tena ifanye kazi hiyo katika viwango vya kimataifa, kwa sababu kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), wanatengeneza ramani ya kujua fursa za kuwekeza zinazopatikana katika vijiji ili tuwe na taswira kubwa na kuja na mradi wa ‘One Village, One Product Factory”, ikiwa na maana ya Kijiji kimoja na bidhaa moja ili kutoa fursa za kiuchumi.

“Sisi kama mkoa, tuliwajua ESRF , lakini kimsingi TVP ndio waliofanya kazi”

“Tunawashukuru ESRF kutuletea watu wenye kufanya kazi katika viwango vya juu vyenye ubora,”

“Kuna watu walishawahi kuomba kazi hapa wakisema wao ndio waliokuwa wametengeza hii documentary kutokana na TVP kutotajwa Katila ile documentary kama ndio walifanya kila kitu,”

“Lakini baada ya kunitembelea ofisini kwangu, nimejua nyie ndio wahusika, nawapongeza sana kwa hii kazi nzuri,” Mtaka aliiambia crew ya TVP, ambayo ilikwenda mkoani Simiyu kwa ajili ya   kutengeneza documentary za video na Makala za magazeti kwa ajili ya kampeni ya taifa ya serikali ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ mama wajawazito na Watoto wachanga.

BAADHI YA KAZI AMBAZO TRUE VISION IMEZIFANYA

TVP ni kampuni kongwe nchini katika kutengeneza documentary na matangazo ya video na radio, ikiwa imefanya kazi ya miradi kadhaa mikubwa ikiwemo na taasisi kama World Bank, UNICEF – Walinde Watoto,  DTB Bank,CARE Tanzania Tanapa,  Ansaf Tanzania BRN Gas Project, Uhamiaji Tanzania – E-Permit/E-Visa, Mamlaka ya Ngorongoro, Trade Mark East Africa (One Stop Border Posts), SHUGA Radio, Air Tanzania, matangazo ya Tafakari, eGA Agancy(Wakala wa serikali Mtandao Tanzania) NHIF, Msongola City, Elimu ya Afya ya Uzazi (TAwla), pamoja na makala ya ‘Huyu Ndio Magufuli’ na Miaka Miwili ya Magufuli ya Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, DataVision-TACIP(Tanzania Art and Craft Identification Project na Tanzania Tourism Board (TTB) miongoni mwa nyingine nyingi.

Simiyu Regional Commissioner, Anthony Mtaka