Kiwango cha Ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania kinaonyesha kukua kwa kiasi kikubwa kulingana na ripoti ya utafiti ya mwaka 2009 ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF.

Takwimu

Takwimu zinaonyesha karibu wasichana 3 kati ya 10 na mvulana 1 kati ya 7 wameripoti kutendewa walau tukio moja la ukatili wa kijinsia kabla ya kutimiza umri wa miaka 18. Karibu asilimia 6 ya wasichana wamelazimishwa kujamiiana kabla hawajatimiza miaka 18.

Takribani robo tatu ya wasichana na wavulana wameripoti kufanyiwa ukatili wa kimwili kabla ya kutimiza miaka 18. Karibu wasichana 6 kati ya 10 na wavulana wameripoti kufanyiwa ukatili wa kimwili na ndugu na 1 kati ya 2 na waalimu.

SOMA ZAIDI:

Utekelezaji wa Mradi wa Sports For Children and Youth Empowerment

Kwa kuliangalia suala hilo kwa jicho la pili, shirika la Plan International kwa kushirikiana na Right to Play waliamua kuzindua mradi maalumu wa Sports For Children and Youth Empowerment katika kuwajengea uwezo watoto na vijana ili kuweza kutambua haki zao na kushiriki katika kulinda na kutetea haki za watoto.

Ukatili dhidi ya watoto

Michezo ndio mbinu na jukwaa kubwa lililotumika katika mradi wa Sports for Children and Youth empowerment. Ikiwa kama sehemu ya kuwaelimisha watoto na mbinu ya kuweza kuwafikia wanajamii mbalimbali.

Wakiwa kwenye shule mbalimbali wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani. Plan international walifanikiwa kutumia michezo na mbinu mbalimbali katika kuwajengea uwezo watoto Mashuleni. Ikiwa na lengo la kupunguza kiasi cha ukatili dhidi ya watoto.

Kupitia michezo Mashuleni, Plan International ilifanikiwa katika kupunguza mimba za utotoni hasa mashuleni pamoja na kupunguza hali ya utoro mashuleni.

Plan International kwa kushirikiana na Right to Play pia ilifanikiwa kuwajengea uwezo watoto mashuleni kupitia michezo. Ilitumia michezo kwa kuwaelimisha kuhusiana na haki mbalimbali za watoto.  Zikiwemo hali ya kulindwa, kuheshimiwa, kupata matibabu pamoja na haki ya kucheza.

True Vision Production (TVP) kama mdau pia ndio chombo maalumu kilichotumika katika kusambaza ujumbe huu kupitia njia mbalimbali kama vile kupitia Makala zilizoandaliwa kutokana na mradi huo.

TVP pia, kama mdau kwenye masuala yote ya kijamii inakupa nafasi ya kushirikiana nayo katika miradi mbalimbali ya kijamii. Katika uaandaaji wa Makala na video mbalimbali zenye kuelimisha na hata kuburudisha. Hii ni kwa lengo la kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira katika njia ya kifanisi zaidi.