Mpaka kufikia Mwaka wa 2030, inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 75 ya idadi ya watu wa Afrika Mashariki itakuwa chini ya umri wa miaka 34, na ni walio kwenye ajira na wasio kwenye ajira.Tayari nchini Tanzania, asilimia 70 ya idadi ya watu wako chini ya umri wa miaka 35, na tunakabiliwa na changamoto kubwa kulingana na idadi hii kubwa ya vijana ambao wanaonekana wametengwa na huduma mbalimbali kama vile ajira, masuala ya fedha pamoja na maisha bora.

Tanzania kwa sasa inajitahidi kufikia Maono ya Mapango wa Maendeleo wa 2025 ili kuwa nchi ya kipato cha kati. Athari nzuri katika suala la uboreshaji wa hali ya maisha kutokana na idadi ya jumla ya watu kwamba mafanikio hayo yanapaswa kuleta, inategemea uwezo wa kutafsiri kasi ya ukuaji wa uchumi katika kupunguza umasikini na kufanikiwa.

Vijana wanajitahidi kuondokana na umasikini kama inavyoakisiwa na takwimu za asilimia 82.% ya vijana walio katika ajira zisizo rasmi, ambayo huongezeka hadi 93.6% kwa vijijini. Kukabiliana na hili, Shirika la Maendeleo la Uholanzi la SNV lilianzisha programu ya fursa ya Ajira ya Vijana (OYE) nchini Tanzania, Msumbiji na Rwanda.

SOMA ZAIDI:

UTEKELEZWAJI WA MRADI WA OYE WA UFUNGAJI WA MFUMO WA SOLAR

Nchini Tanzania, mradi huu una lengo la kuboresha mapato na maisha ya vijana 18,000 wa vijijini wenye umri wa kati wa miaka 18-30 walio nje ya mfumo wa elimu, kwa kuunda fursa za ajira katika kilimo, nishati mbadala pamoja na usafi wa maji na mazingira

Bwana Donald Beatus Mlolwa, ni mkaazi wa kijiji cha Kigwa , kata ya Kigwa Mkoani Tabora. Yeye ni moja ya wanufaika wa mradi wa OYE wa ufungaji wa mifumo ya Solar ikiwa kama njia ya kuzalisha nishati mbadala kwa maeneo ya vijijini.

Kupitia mradi wa OYE, bwana Donald anasema amenufaika kwa kiasi kikubwa hasa katika kuboresha maisha yake kutokana na kumpatia ujuzi uliompelekea kupata ajira ya kuingiza kipato kinachoweza kuendesha maisha yake.

Kabla ya kuingia kwenye mradi huu wa ufungaji wa mifumo ya Solar, bwana Donalad anasema OYE walimpatia semina maalumu ya ufungaji wa mifumo hiyo ya Solar kabla ya kuanza kufanya kazi ambapo baadae ilimpa hali ya kuongeza ujuzi wa kufunga mifumo ya satelite ya kunasa mawimbi ya television.

Kabla ya kuja mradi wa OYE maisha yangu yalikuwa ni hafifu, nilivyojiunga na mradi wa OYE nilichagua mradi wa ufungaji wa mfumo wa solar, baada ya kupokea mafunzo mimi na wenzagu tulirudi kijijini na tukaanzisha kikundi”-Anasema Donald

Bwana Donald sasa yupo kwenye kikundi maalumu walichokianzisha kwa ajili ya shughuli za ufungaji wa mifumo ya Solar kinachoitwa Kigwa Youth Solar Entriprises na kupitia mradi huo amefanikisha kujenga nyumba yake ambapo pia washirika wenzako walimsaidia katika kufanikisha jambo hilo.

Maisha ya Donald sasa si kama ya zamani, kutokana na kipato kilichotokana na shughuli za ufungaji wa Solar, sasa ameweza kuanzisha mradi wa Unga wa lishe ambao unatengenezwa na mke wake na kisha kuusambaza sehemu mbalimbali.

True Vision Productions kupitia Ubalozi wa Uswisi chini ya wakala wa Maendeleo na ushirikiano Uswisi, ndio waliofanikisha kuandaa makala mbalimbali za wanufaika wa mradi wa OYE kupitia SIDO nchini Tanzania.

Mradi wa OYE unaotekelezwa na SNV kwa kushirikiana na Foundation ya Mastercard na Shirika la Uswisi la Maendeleo na Ushirikiano Uswisi, umekusudia kuwafikia vijana wasiokuwa na ustawi wa vijijini wenye umri wa miaka kati ya miaka 18 na 24, angalau 40% kati yao ni wanawake wenye umri wadogo.