Linapokuja suala la kazi, kila mmoja wetu ana njia zake za kukamilisha kazi yake. Lakini ni wazi kuwa kundi lolote la watu wenye kufanikiwa huwa wana tabia zinazolingana. Mafanikio ya kazi nzuri daima ujengwa na wafanyakazi wenyewe katika ya dhana ya uwajibikaji kama ilivyo vya True vision Production.

True Vision Production, ni kampuni inayojishughulisha na uzalishaji wa vipindi mbalimbali vya Televisheni, radio, lakini hata uzalishaji wa matangazo mbalimbali ya biashara na yasiyo ya biashara, Makala pamoja na uandaaji wa kampeni na miradi mbalimbali kupitia mashirikia ya serikali, sekta binafsi na hata NGO.

Ukweli ni kwamba kwa kiwango kikubwa True Vivision imejipambanua katika kutoa kazi zenye ubora na zenye kukidhi hitaji la adhira yake. Lakini mfanikio haya hayaji tu hivi hvi bali uchochewa na vitu mbalimbali. Baadhi ya vitu hivyo na kama,

Timu ya TVP ikiongozwa na Mkurugenzi wake, Bwana David Sevuri kwenye mkutano wa kiuchumi (TANZANIA ECONOMIC UPDATE-‘Human capital: The Real Wealth of Nations’ ) ambao umeandaliwa na World Bank.

SOMA ZAIDI:

Siri za mafanikio ya kazi nzuri

  1. Uzoefu na Ujuzi

True Vision Production (TVP), inaundwa na timu yenye uzoefu na ujuzi wa kazi wa zaidi ya miaka 15 katika uwanja wa video production. Uzoefu huu unajumuisha pamoja na kufanya kazi mbalimbali na katika maeneo mbalimbali pamoja na kujitolea.

  1. Utendaji kazi wa pamoja (Team work)

Team work ndio kigezo cha kazi bora. Kwa muda wote TVP imekuwa ikifanya kazi zake kwa umoja. Hii ndio imekuwa chachu hasa ya kufanya kazi katika weledi wa hali ya juu kabisa.

  1. Uwepo wa Vitendea kazi vyenye sifa na uwezo mkubwa

Bila kusita, uwepo wa vitendea kazi vya kutosha na vyenye sifa hufanya kazi kuwa maridadi zaidi. Ubora wa kazi pamoja na picha na video nzuri utokana na vifaa bora zaidi vyenye kukidhi haja katika mazingira ya aina yote. Vifaa ndio msingi mkubwa wa kazi yenyewe. Hivyo bila kusita TVP iliamua kujiwekeza katika eneo hilo.

Ipo miradi, kampeni na makala mbalimbali ambazo zimefanywa na True vision Production ambazo unaweza kuzitofautisha na kazi nyingine kwa ubora wake. Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA.