Ikiwa una lengo la kukuza biashara yako au huduma unayotoa au labda kuongeza ufahamu wa bidhaa yako au hata kuelezea jinsi bidhaa mpya inavyofanya kazi, matumizi ya “Corporate Video” (Video za kampuni) inaweza kuwa njia bora na sahihi kwenye biashara yako.

Corporate Video zinaleta ufanisi mkubwa kwenye biashara na hatimaye kukuza mapato yako kwa zaidi ya 49% kwa mwaka. Hii ni zaidi ya mashirika, kampuni na hata biashara ambazo hawatumii njia hii.

Video za kampuni (Corporate Video) zinaweza pia kuwa chombo kikubwa cha kuwasilisha jambo lenye uzito kwa njia nyepesi na yenye afya. Jambo hili linaweza kuwa lenye kuelezea kuhusu huduma fulani au kuhusu bidhaa, matumizi yake na hata upatikanaji wake.

SOMA ZAIDI:

Corporate Video (Video za kampuni ni nini?

Video ya kampuni inahusu aina yoyote ya maudhui ya video yasiyo ya matangazo. Maudhui yaliyoundwa na kutumiwa na biashara, kampuni, au shirika fulani.

Siku za hivi karibuni maudhui ya video ya kampuni yamekuwa yakichapishwa mtandaoni. Na hata kuchapishwa kwenye ukurasa wa tovuti ya kampuni na kusambazwa pia kupitia Mitandao ya kijamii au barua pepe za kimasoko (Email marketing).

Utafiti uliofanywa na kampuni moja ya uzalishaji wa Video za masoko nchini Uingereza, Wyzowl kwa mwaka 2017, unaonyesha kuwa 81% ya wafanya biashara hutumia Corporate video kama dhana ya kutangaza biashara na huduma zao. Huku kati yao,

  • 99% ambao walikuwa wanatumia Corporate video waliendelea kutumia njia hiyo (Promotional Video)
  • 85% walithibitisha kuwa Corporate video ndio njia pekee ya kimkakati ya masoko kwenye biashara zao
  • 82% waliweka mipango ya kuendelea kutumia njia hiyo kwa mwaka uliofuata
  • 78% walisema Corporate Video inawapa ufanisi katika kuchanganua marejesho ya walichowekeza. (Return on Investment, ROI.)
Mfano wa Corporate Video iliyofanywa na True Vision Production.

True Vision Production (Video Production Company in Tanzania) imekuwa kwa kipindi kirefu ikijihusisha na kuandaa Corporate za mashirika na kampuni mbalimbali. Kukiwa na ubunifu wa hali ya juu, TVP imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuaandaa Video za kampuni zenye kuleta ufanisi.

Hivyo basi ni wazi kama kampuni au shirika una nafasi ya kuangalia fursa ya kuwapa jamii kile unachokifanya katika njia iliyobora. Kwa ajili ya kupata Video Corporate zenye ubora, tafadhali wasiliana nasi kwa kubonyeza HAPA.

Mfano wa II wa  Corporate Video iliyofanywa na True Vision Production.