Moja ya malengo ya maendeleo ya Milenia yaliyowahi kuwekwa ni pamoja na usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake. Lengo hili lilikuwa linataka wanawake au akina mama wapewe fursa sawa katika nyanja zote ikiwamo kiuchumi, kisiasa na hata kijamii.

Licha ya malengo hayo kufikia ukomo wake 2015, lakini bado juhudi zinafanyika ili kuwakomboa akina mama na kuwahusisha katika mfumo mzima wa uzalishaji. Na hii ndio zana ya fursa sawa katika kukuza uchumi.

True Vision Production imetembelea akina mama wajasiriamali kutoka katika kijiji cha Bunazi, Mkoani Kagera Km 18 kutoka kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda, Mutukula ambao wamefikiwa na mafunzo ya Ujasiriamalia kutoka kwa TradeMark East Africa.

Mafunzo ya TradeMark yalivyoleta tija kwenye Shughuli zao

Kwa kutumia vikundi ambavyo wamevianzisha. Akina mama hao wajasiriamali wanaojihusisha na Kilimo hai cha Mahindi ya njano, Maharage ya njano, Maharage ya Soya, Karanga kwa kutumia mbolea za asili wamekuwa wakipokea semina mbalimbali kutoka kwenye mashirika kama vile Trade Mark East Africa kuhusiana na ujasiriamali.

Trade wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali kwa vikundi hivyo vya akina mama katika Nyanja mbalimbali kama vile,

  • Kutafuta Masoko kwa kutumia Mtandao
  • Jinsi ya kuvuka mpaka wa Mutukula kwa njia ya halali kupitia Uhamiaji
  • Kutambua kuhusu TFDA na TBS ili kuweza kujua thamani na viwango vya ubora wa bidhaa zao
  • Namna ya kufungasha bidhaa zao kwa ustadi (Packaging)
  • Usajili wa bidhaa zao
  • Kuhusu tozo na kodi mbalimbali kutoka TRA

akina MAMA

Kupitia mafunzo hayo wanayoyapata imewasaidia kutambua namna ya kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao yao kwa kutengeneza Unga lishe wa maharage ya soya (Soya beans) na mahindi ya njano (sweet Corn) lakini pia kufanya biashara zao kuwa rasmi.

“Zamani tulikuwa tunajiendea tu, tulikuwa hatujui hata kama huo uhamiaji upo! Ukifika pale unaangaalia unasema hapana, unapita huko vichochoroni”-alisema Bi Paskazia Sebastian, mjasiriamali wa Mutukula.

akinama wa Bunazi

Ili kuweza kuuza bidhaa zao wakati mwingine akina mama hao umepeleka bidhaa kwenye maonyesho mbalimbali kama vile maonyesho ya Jua kali ya kampala na kuza bidhaa zao kwa bei ya faida. Na wakati mwingine huvusha bidhaa zao hadi maeneo ya karibu ya nchi ya Uganda walahu kwa mara moja kwa mwezi.

Mutukula ni mji ulio mpakani mwa Tanzania na Uganda. Na ni kiunganishi kikubwa cha biashara hususani kwa nchi hizi mbili yaani Tanzania na Uganda. Takwimu zinaonyesha kuna zaidi ya magari 418 hupita katika eneo la mpaka huo kwa siku, huku magari kama Malori uchukua muda mrefu kukaa katika eneo hilo.