Jitambu. Tambulika. Inalipa, ni kauli mbiu inayotumika kwenye mradi wa TACIP wa utambuzi wa wasanii wa sanaa za ufundi nchini. Mradi huu unalengo la kuwaunganisha wasanii wa kazi za sanaa za ufundi ili kuweza kutambulika na kujitambua pia kuwa sanaa za ufundi zinzweza kuingiza kipato kikubwa kama tu walanguzi wanaweza kupungua kwenye sekta hiyo.

Sanaa ni ufundi anaoutumia mwanadamu ili kuwasilisha fikra au mawazo yaliyo ndani ya akili yake. Kwa maana nyingine, sanaa ni uzuri unaojiibua katika umbo lililosanifiwa.

Kutokana na kukosa thamani kwa tasnia hii kwa muda mrefu, DataVision International wakishirikiana na Tanzania Federation of Craft and Arts (TAFCA)  pamoja na True Vision Production imeamua kuja na mradi maalumu wa utambuzi wa wasanii wa Sanaa za ufundi, TACIP (Tanzania Arts and Craft Identification project) .

SOMA ZAIDI:

Lengo kuu hasa la mradi huu ni

  1. Kupunguza walanguzi ambao wanajitokeza katikati ya biashara ya sanaa za ufundi kabala ya kufika kwa mteja
  2. Kuwapa thamani wasanii kwa kuwaunganisha na soko/mteja moja kwa moja ili kuondoa ombwe lililopo kati ya msanii na mteja pamoja na kumleta msanii karibu na soko.

“Kuna kikapu kimoja kimeuzwa dola 3,000 ambapo ukienda Bagamoyo au Nangomba watu wananunua kwa shilingi elfu tano tu”-Rais TAFCA

Kupitia mradi huu wa TACIP, ni wazi kama wasanii watauunga mkono basi wataenda kubadilisha maisha yao kupitia Sanaa za ufundi. True Vision Production kwa kushirikiana na DataVision Internationa pamoja na TAFCA imemulika kwa kina shughuli nzima za wasanii wa Sanaa za ufunundi na kuaandaa makal fupi za mchakato wa mradi huu ambao dhana yake inabebwa na ujumbe usemao JITAMBUE. TAMBULIKA. INALIPA