Kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana kwa nchi za Tanzania, Rwanda, na Msumbiji, ni mara 2-3 zaidi kuliko cha watu wazima. Lakini pia kuna kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira kwa wanawake wenye umri mdogo. Hii ni kwa mujibu wa takwimu za shirika la kimataifa lisilo la kibiashara la Maendeleo la nchini Uholanzi (SNV)

Zaidi ya hayo, viwango vya umaskini katika nchi hizi tatu vipo kati ya 45% hadi 68%, kulingana na Benki ya Dunia. Wengi wa vijana wa vijijini wanategemea ajira zilizo katika mazingira ‘hatarishi’ na kilimo kisichokuwa cha kibiashara (kwa ajili ya kulisha familia) ili kujiendeleza.

Hii ni pamoja na kuwa na kazi zisizo rasmi za kujitegemea bila ya kuwa na mapato imara au fursa ya maendeleo ya kitaaluma au ukuaji wa muda mrefu.

Hali hiyo inafanya vijana wengi sasa kukimbilia mijini (hasa miji mikuu) kwa ajili ya kutafuta ajira, wakidhani ndio suluhisho la mahitaji yao ya kimaisha.

Serikali pamoja na taasisi mbalimbali zisizo za kibiashara zimekuwa zikipambana katika kutafuta mwarobaini wa tatizo hilo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana hasa wanaoishi maeneo ya vijijini.

Kwa kukabiliana na hili, Shirika la Maendeleo la Uholanzi la SNV lilianzisha programu ya fursa ya Ajira kwa Vijana (OYE) nchini Tanzania, Msumbiji na Rwanda.

SOMA ZAIDI:

UTEKELEZWAJI WA MRADI WA OYE

SNV inatekeleza mradi wa OYE (Opportunities For Youth Employment) nchini Rwanda, Tanzania na Msumbiji kwa lengo la kuboresha maisha ya vijana wa vijijini, 27,050 wakiwa nje ya mfumo wa elimu mashuleni kuwafikia kwa njia ya mafunzo ya ujuzi ili huchochea matarajio yao wao wenyewe na na kuwatia moyo katika ushiriki wa kilimo cha ndani, uzalishaji wa nishati mbadala, kushiriki katika biashara na kuwa na kipaumbele cha usafi wao binafsi (muonekano mzuri).

Nchini Tanzania, Shirika la viwanda vidogo vidogo (SIDO) limekuwa likitekeleza mradi huu, majukumu yake yakiwa ni kutafuta vijana na kuwafundisha mafunzo mbalimbali kulingana na matakwa ya Mradi wa OYE.

Emmanuel Joseph, mkaazi wa Dodoma mjini nchini Tanzania, ni mmoja wa wafaidika wa mradi wa OYE, ambaye maisha yake yameonekana kuwa tofauti na kipindi cha nyuma mara tu baada ya kujiunga na Mradi wa OYE. Mradi ambao umejikita katika utengenezaji wa viatu vinavyotokana na ngozi.

Joseph anasema SIDO ndio waliomuwezesha kupata mafunzo ya ngozi ambayo baadaye yamlisaidia kukutana na vijana wengine waliopata mafunzo kama hayo na kuamua kuanzisha kituo chao maalumu kwa ajili utengenezaji wa viatu vya ngozi.

“Niliwajua OYE kupitia SIDO ambao walikuwa wanatafuta vijana kwa ajili ya kuwapa mafunzo mbalimbali yakiwemo ya ngozi, chakula, lakini mimi nilipendelea mafunzo ya ngozi”- anasema Joseph.

Kwa sasa Joseph yupo kwenye kikundi maalumu cha utengenezaji wa ngozi walichoanzisha yeye pamoja na vijana wengine wanaotoka kwenye mradi wa OYE wa ngozi kinachojulikana kama ‘4U Leather Product’. Kikundi ambacho bwana Emmanuel anasema walianza na mtaji wa shillingi laki mbili.

Joseph sasa ametumia ujuzi wake kwa kuwafundisha vijana wengine ambao wengi wao walipendezwa kujiunga na kikundi chake na kuendelea kufanya kazi pamoja.

Joseph anasema wanauza bidhaa zao sio Dodoma tu, bali pia katika mikoa yote nchini Tanzania, nan chi jirani ya Uganda, lengo likiwa kuzifikia nchi za Afrika Mashariki kama vile Burundi na nyinginezo.

WAWEZESHAJI NA WASHIRIKA WA MRADI WA OYE

Mradi wa OYE unaotekelezwa na SNV kwa kushirikiana na Foundation ya Mastercard na Shirika la Uswisi la Maendeleo na Ushirikiano. Ukiwa unakusudia kuwafikia vijana wasiokuwa na ustawi wa vijijini wenye umri wa kati ya miaka 18 na 24, angalau 40% kati yao ni wanawake wenye umri wadogo.

True Vision Productions (Video Production company in Tanzania) kupitia Ubalozi wa Uswisi chini ya wakala wa Maendeleo na ushirikiano Uswisi, ndio waliofanikisha kuandaa makala mbalimbali za wanufaika wa mradi wa OYE kupitia SIDO nchini Tanzania.