Wiki ya Asasi za kiraia (Azaki) 2019 imemalizika mapema wiki iliyopita ya tarehe 8 Novemba, 2019 mjini Dodoma. Wiki hii ilianza kuadhimishwa mnamo tarehe 4 novemba, 2019 huku ikibeba ujumbe wa mahusiano na ushirikiano wa dhati kwa wadau wote wa maendeleo nchini.

Licha ya kufanyika kwa midahalo mbalimbali inayojadili sera mbalimbali za maendeleo pamoja na asasi za kiraia. Wiki hii ilibeba dhana kubwa ya kuimarisha uhusiano baina ya watendaji wa serikali na wale wa sekta binfasi.

Mkurugenzi Mtendaji Wa The Foundation For Civil Society , Francis Kiwanga ( kushoto) akisalimiana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu katika maadhimisho ya wiki ya Azaki 2019 mjini Dodoma.

SOMA ZAIDI:

Yapo mambo kadha ambayo ndio yametajwa kama mhimili au malengo mahususi ya Kuimarisha mahusiano baina ya wadau wakuu wa maendeleo. Mambo haya hasa yamelenga kuongeza na kuimarisha mahusiano baina ya,

  1. Azaki na Serikali

Hii itasaidia katika kuweza kuonyesha mchango wa Sekta ya Azaki kwenye kuchangia maendeleo

  1. Azaki na Bunge

Lengo kubwa hasa likiwa ni kuonyesha ushiriki na mchakato wa Azaki katika michakato ya kisera.

  1. Azaki na Sekta Binafsi

Hapa lengo kuuu hasa ni kuweza kuongeza mchango wa kifedha na kiufundi katika shughuli za kimaendeleo

  1. Azaki kwa Azaki

Kuweza kuimarisha uhusiao baina ya azaki kwa azaki ili kuweza kuwajengea sauti ya pamoja na kuwawezesha kufikia malengo ya kuleta maendeleo kama kikundi kimoja.

  1. Azaki na Wananchi

Lengo kuu ni kuwawezesha wananchi kuwa na sauti hasa wale walio pembezoni ili kuweza kuwa na ushawishi katika michakato ya utawala katika ngazi zote nchini.

Wiki hii ya ya Asasi za Kiraia nchini Tanzania, ambayo imeandaliwa kwa mara ya pili mfululizo na The Foundation For Civil Society, iliudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na sekta binafasi.

Baadhi ya viongozi hao ni pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi pamoja na Mtendaji Mkuu wa The Foundation For Civil Society (FCS), Bwana Francis Kiwanga.

Asasi na taasisi mbalimbali za maendeleo kama vile UN Women, Oxfam, Twaweza, Policy Forum, Msichana Initiative, UNA Tanzania, Sikika, Tango, Tanganyika Law Society na wengine wengi ni sehemu pia ya washiriki.

True Vision Production (TVP) kwa kutumia weledi wake ilikusanya matukio yote muhimu kwa kutumia video, picha za mnato na kutengeneza clip ndogo ndogo za siku kwa ajili ya wadau wa mitandao ya kijamii (social media) ili kushea katika platform mbalimbali kama vile Twitter, Instergram, YouTube na Facebook.