Kimsingi rushwa ya ngono ni moja ya matendo ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia unaowaathiri hasa wanawake mashuleni, makazini na sehemu mbalimbali. Unyanyasaji wa namna hii umekuwa ukiripotiwa mara kwa mara na wahusika licha ya kuwepo pia wimbi kubwa la wale wanaoishindwa kutoa taarifa. Serikali pamoja mashirika mbalimbali kama vile TGNP mtandao yamekuwa yakifanya juhudi kubwa za kukomesha tatizo hili.

Kufuatia kukithiri kwa matendo hayo ya ukatili ya rushwa ya ngono, akinamama wameamua kupaza sauti zao. Baadhi ya akina mama walioudhuria kwenye tamasha la 14 la kijinsia walioneka na mabango mbalimbali ya kupinga rushwa ya ngono. Baadhi ya mabango hayo yalikuwa yanasome hivi,

“Paza sauti kudhibiti rushwa ya ngono. Rushwa ya ngono ni adui wa haki, dawa ni kuikomeshwa

“Tanzania bila rushwa ya ngono inawezekana, pata ujasiri kumtaja anaeomba rushwa ya ngono”

Tamasha la jinsia la 14 limefanyika mwishoni mwa mwezi Septemba, 2019 likibeba ujumbe unaosema “Wanaharakati wa kijinsia mbioni kubadilisha Dunia”. Tamasha ambalo lilienda sambamba na maadhimisho ya miaka 25 ya TGNP pamoja na azimio la mpango kazi wa Beijing uliokuwa na lengo la kupambana na ukatili wa kijinsia Duniani. True Vision Production walipata nafasi ya kurusha mubashara (Live) tamasha hili kupitia mitandao mbalimbali.

Tamasha hilo liliudhuriwa na Mama Getrude Mongella, spika wa zamani wa bunge la Afrika, Spika wa zamani wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Anna Makinda, Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Faustine Ndungulile, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Anders Sjoberg pamoja na viongozi na wadau mbalimbali.